EN | SW

Mpango wa Hack Club Athena

Kuja tucode tarehe 8 Machi, kutoka saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni, pale Nairobi Game Development Centre.

Jisajili

Jua ni nini?

Jua ni event ya wasichana kucode. Tunakuja pamoja, tunatengeneza projects, tunalearn skills mpya, na tunajienjoy! Hata kama hujawahi code, tutakufunza! Unaweza tengeneza website yako ya kwanza ama game kali.

Events za Kitambo

Workshops na Tracks

Sprig

Hapa utafunzwa kutengeneza games za 2D kwa kutumia JavaScript.

Utangulizi wa Web Dev

Hii ni workshop enye unaweza kufunzwa kutengeneza website yako mwenyewe.

Maswali

Nani anaweza kuja?

Hii event ni kwa wasichana wenye wako na miaka 13-17 wenye wanataka kujua kucode!

Na kama sijawahi code?

Usijali, tutakuwa na mentors na workshops za kukusaidia hatakama hujawahi code.

Nahitaji kulipa?

Zi; ni free!

Nilete nini?

Wewe na laptop tu! Kama huna laptop, tuambie mapema tutakupangia

Event inafanyika wapi?

Nairobi Game Development Centre, Diamond Plaza, ghorofa ya 6, Nairobi.

Nikona maswali zingine

Tuma email hapa: zenab@hackclub.com